Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mnzava wakati wa uzinduzi wa mradi wa kikundi cha vijana Tumaini kilichopo katka Kata ya Itete kijiji cha Alabama kinachojishughulisha na kilimo pamoja na usafirishaji wa mizigo kwa kutumia powa tila.
"Mwenge wa Uhuru umeridhika kwamba mnafaifanya kazi hii vizuri ya kuwawezesha Vijana na tuko tayari kufanya uzinduzi wa mradi huu, na hasa ukizingatia Vijana hawa wamewezeshwa na Halimashauri husika "amesema Godfrey Mnzava.
Mapema akisoma taarifa ya mradi huo Katibu wa Kikundi cha Vijana Tumaini Hepinesi Petro amesema gharama za mradi huu wa powa tila ni shilingi milioni 19,967,000 ambapo milioni 14, 967,00 ni mkopo kutoka aslimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri na shilingi milioni 5,000,000 ni michango ya wanakikudi.
Sambamba na hilo Hepinesi amesema kuwa mradi huo umekua mkombozi katika shughuli za kilimo Wilayani Malinyi ambapo Powa tila hiyo inauwezo wa kulima ekari 3 kwa siku,na imewawezesha wanakikundi hao kuanzisha biashara ndogondogo zinazowasidia kujiiingizia kipato binafsi.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa Wilayani Malinyi leo April 25, utapitia miradi mitano yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 400 na unakimbizwa kwa umbali wa kilomita 194 ndani ya Wilaya ya Malinyi mpaka utakapokabidhiwa katika Halmashaurri ya Mji Ifakara Kesho April 26, 2024
Mpaka mwandishi anapoandika habari hii tayari Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa kikundi cha Vijana Tumaini umeona mradi wa miche na mazingira uliopo Kata ya Itete Kijij cha Njiwa juu na umezindua mradi wa ukarabati wa jengo la mionzi katika Kituo cha afya Mtimbira.
"KAULI MBIU:TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA UJENZI WA TAIFA ENDELEVU"
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.