April 11, 2024 Jopo la Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe.Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Godfrey Kasekenya pamoja na Mawaziri wengine wamefanya ukaguzi wa miundombinu ya barabara katika Wilaya ya Malinyi kwa kutumia usafiri wa helikopta.
Hatua hiyo imekuja siku 6 baada ya Mbunge wa Malinyi Mhe. Antipasi Mgungusi kuwasilisha Bungeni kilio cha Wakazi wa Malinyi kuhusu changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambazo zimeharibiwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Malinyi.
Mapema April 5, 2024 Mhe. Mgungusi alieleza Bungeni kuwa athari za mafuriko Wilayani malinyi ni kubwa sana kuliko inavyoonekana katika mitandao na hivyo kuiomba Ofisi ya Waziri Mkuu kulichukulia jambo hili kwa uzito na kuongeza kuwa Wakazi wa Malinyi wanahitaji msaada wa haraka.
Akizunguza na Wananchi waliokua wanausubiri ugeni huo eneo la njia panda, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amesema kuwa ugeni huo umeshindwa kutua katika eneo lililokusudiwa njia panda pamoja na maeneo mengine kutokana na maeneo mengi ya Malinyi kuwa katika hali ya ubichi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.