Leo Februari 15, 2024 Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastia Waryuba amezindua chanjo ya Surua Rubella katika zahanati ya Malinyi Wilayani Malinyi kwa niaba ya zahati na vituo vya afya vyote vilivyopo Wilayani Malinyi.
"Chanjo hii ni salama, muwe mabalozi kwa Watu wengine, pasiwepo na mtu mwingine wa kuleta imani potofu juu ya chanjo hii" amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
Mhe Sebastuan Waryuba amewataka Wazazi / Walezi wote Wilayani Malinyi kuwapeleka watoto kwenye Zahanati, na Vituo vya afya vilivyopo karibu yao ili kupata chanjo hiyo dhidi ya ugonjwa wa surua rubela.
Chanjo ya surua rubela inayotolewa kwa watoto kuanzia miezi 6 hadi miaka 5 ina dhumuni la kujenga afya bora kwa Watoto, Kwa mujibu wa Mratibu wa chanjo Wilayani Malinyi ndugu Eliesikia Mbwambo jumla ya Watoto 99 kuanzia miezi 6 hadi miaka 5 wamepatiwa chanjo hiyo leo Februari 15, 2024 katika Zahanati ya Malinyi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.