Novemba 23, 2023
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na kuwahusisha Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watumishi wengine.
Imeelezwa kuwa Mfumo wa Watumishi portal ni kwaajili ya uombaji wa uhamisho kutoka Taasisi moja kwenda Taasisi nyingine ambapo Mfumo wa Hazina Portal ni kwaajili ya kuona hati ya mishahara na uombaji wa mikopo ya Benki.
Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu ndugu Gasto Silayo amewasisitiza Watumishi wote kujiunga katika mifumo hiyo na kuongeza kuwa kupitia mfumo wa Watumishi Portal Mtumishi anaweza kujihudumia mwenyewe akiwa mahali popote kwa njia ya mtandao na kupata baadhi ya huduma kama vile kupata hati ya mshara.
Sambamba na hilo, Imeelezwa kuwa Mafunzo katika ngazi ya Tarafa yanatarajiwa kufanyika hivi karibuni na yatawahusisha Watumishi kutoka sekta ya elimu, sekta ya afya, Watendaji wa Kata na Vijijiji.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.