Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Makamu Mwnyekti wa Halmashauri ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Sofi Mhe. Lucasi Mgomahenga imefanya ziara katika Shule mpya ya Sekondari Kiswago lengo likiwa ni kukagua maendeleo ya ujenzi katika shule hiyo.
Shule mpya ya Sekondari Kiswago imejengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa SEQUIP ambapo kwa sasa ujenzi huo umekamilika kwa 90% na umegharimu jumla ya shilingi milioni 477,479,197,.45 kati ya shilingi milinoni 528,998,425 zilizopokelewa kutoka Serikali kuu ambazo zimeweza kujenga jengo la Utawala, Madarasa 8, Ofisi 2, jengo la Tehama, Maabara ya Kemia na Biolojia, Maabara ya fizikia Matundu ya vyoo kwa Wavulana na Wasichana.
Taarifa iliyosomwa mbele ya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imeeleza kuwa ujenzi wa shule hiyo katika eneo la Kiswago ulilenga kutatua changamoto za Wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu yanayohatarisha zoezi la ufundishaji na ujifunzaji na kuongeza kuwa shule mpya ya Sekondari Kiswago ni mkombozi kwa Wanafunzi wa Vijiji vya Salamiti, Langalanga, Mnazi mmoja na Kiswago kwa ujumla waliokua wakitembea umbali mrefu wa kilometa 15 kwenda shule na kurudi nyumbani hali iliyosababisha Wanafunzi kuacha shule na wengine kupata ajali barabara wakati wa kwenda shuleni na kurudi nyumbani.
Sambamba na hilo, Taarifa hiyo imeeleza kuwa mpaka kufikia Januari 2024 shule hiyo ilifanikiwa kupata Waalimu na kupokea Wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa 50%.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.