Mgombea Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bw. Lucas John Mgombahenga ametangazwa mshindi kwenye Uchaguzi mdogo wa Udiwani uliofanyika kata ya Sofi. Uchanguzi huo ulihusisha vyama vinne ambavyo ni ACT-WAZALENDO, CUF, CHANDEMA na CCM ulifanyka ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi, baada ya Diwani aliyekuwepo hapo zamani kupitia CCM kufariki Sunia. Akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bw. Marcelin R. Ndimbwa, alisema Bw. Lucas Mgomahenga alipata kura 2099 kati ya kula halali 3839 na kuwashindwa wagombea wenzake.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.