Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini hali ya barabara baadhi ya maeneo wilayani malinyi imeonekana kuwa ni changamoto hivyo kupelekea magri kushindwa kuendelea na safari zake na kukwama.
Aidha Eneo ambalo linaonekana kuwa ni changamoto zaidi ni MSITU NAMBIGA ambapo mara kadhaa magari hukwama na wakati mwingine abiria kulala hapo hali ambyo ni hatari kiusalama huku wahusika wakilazimika kutumia pumba za mpunga kwa kumwaga barabarani ili kupata hali ya ugumu kidogo kwani tope ni nyingi .
Hata hivyo jitihada mabalimbali zinazidi kufanywa na uongozi wilayani ili kuhakikisha ufumbuzi unapatikana kuweza kutatua changamoto hizo.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.