Wakuliama wanaolima ndani ya skimu ya umwagiliaji itete wametakiwa kuahakikisha kuwa mashamba yote ndani ya skimu yanalimwa kipindi chote cha mwaka bila ya kujali masika wala kiangazi.
Kauli hiyo imetolewa na mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Malinyi Majura Kasika wakati akifunga mafunzo ya 9 kufanyika hapa nchini juu ya kilimo cha umwagiliaji na usimamizi wa rasilimali maji kwa wakulima wa itete na njiwa.
Aidha shughuli hiyo fupi ambayo imefanyika katika ukumbi wa shule ya Bishop Mchonde huku ikijumuisha wakulima hao 30 pamoja na viongozi mbalimbali chini ya Taasisi inayojitegemea na kufadhiliwa na serikali za Kenya Uganda na Tanzania African Institute for Capacity Development (AICAD) .
Majura ameongeza kuwa mafunzo yaliyotolewa ni vyema wakayatekeleza huku waendako na kuwagawia wenzao ambao hawakupata fursa ya kushiriki taaluma hiyo kwani taasisi ya AICAD inaendesha mafunzo ya namna hii ili kuwajengea uwezo wa maarifa wakulima ili waweze kuwa na kilimo chenye tija.
Kwa upande wa mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo bwana …………ameshukuru shirika hilo kwa mafunzo waliowapatia na kuwaahidi kuwa watakuwa walimu bora kwa wengine huku akitoa ushauri kwa wakulima wengine kuacha mazoea ya kilimo cha aina moja cha kutegemea mvua pekee kwani wanapaswa kulima kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mafunzo ya kilimo cha umwagiliaji na usimamizi wa rasilimali maji kwa wakulima wa itete na njiwa wilayani Malinyi yalifunguliwa rasmi 06 November mwaka huu na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Marcelin Ndimbwa kuhimishwa 17 November na mkuu wa wilaya Mjura Kasika.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.