Maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti wilayani Malinyi yenye kauli mbiu "PANDA MITI, TUNZA MITI UPATE NISHATI" imeadhimishwa Shule ya Msingi Nawigo, ikihudhuliwa na mgeni rasmi NDG. LAMECK LUSESA kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Malinyi. Katika siku hiyo Miti 1500 ilipandwa, ikiwa ni Miti 800 iliyopandwa Shule ya Msingi Nawigo, Miti 350 iliyopandwa Shule ya Sekondari Sofi na Miti 350 iliyopandwa maeneo mbalimbali ikiwepo Shule ya Sekondari Kipingo.
Katika maadhimisho hayo Ndg. Lameck Lusesa alisisitiza kuachwa mara moja ukataji Miti holela unaoendelea, hasa Tarafa ya Ngoheranga ambapo ukataji Miti umekithiri zaidi na badala ya ke Wananchi wapande Miti kwa ajili ya manufaa yao na ya Taifa kwa ujumla.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.