Watu wa Kabila la jamii ya wafugaji wamewapiga na kuwajeruhi maeneo mbalimbali ya miili yao wakulima katika wilaya ya malinyi.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo Laurent kidunda ambaye pia ni ndugu wa mmoja wa majeruhi ameeleza kuwa chanzo cha ugomvi huo ni kwamba kabila la wafugaji waliingiza mifugo yao katika mashamba ya wakulima hao na kuanza kulishia mazao.
Aidha mganga wa zamu katika hospitali ya kilutheri lugala mtabibu Daud Magungu amekiri kupokea majeruhi ambao ni Michael kidunda miaka 31 na juma Njaku miaka 32 kutoka kijiji cha lupunga tarafa ya ngoheranga wakiwa na majeraha kichwani na mikononi na kupatiwa matibabu na hali zao zinaenelea vizuri.
Hata hivyo diwani viti maalumu tarafa ya Ngoheranga Prisca Machege ameelezea mkasa huo na kudai kuwa mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi na amelaani vikali vitendo huku akisisitiza ushirikiano ili kuweza kudhibiti kabisa hali hii kwani yaweza pelekea madhara makubwa.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.