: SHIRIKA la Eye Care Foundation lililopo miini Ifakara leo tarehe 13 novemba limetoa vifaa vya matibabu ya macho katika hospitali ya wilaya ya Malinyi vyenye thamani ya shilingi milioni 68.1.
Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Malinyi mbele ya viongozi wa halmashauri hiyo wakiongozwa na mkurugenzi wake mtendaji Hawa Mposi.
Akikabidhi vifaa hivyo,Mratibu wa mradi wa Eye Care Foundation Daniel Wilbard amesema wameamua kutoa vifaa hivyo tokana na uhitaji wa vifaa na huduma katika wilaya hiyo.
Wilbard amesema shirika hilo lipo mjini Ifakara wilayani Kilombero na linafanya kazi katika halmashauri zote nne za wilaya tatu ambazo ni halmashauri za mji Ifakara na wilaya ya mji zilizopo wilayani Kilombero na halmashauri za Ulanga na Malinyi.
Amesema licha ya kutoa vifaa pia wanatoa huduma za macho katika halmashauri hizo na kuahidi kuendelea kutoa huduma katika maeneo hayo kadri siku zinavyokwenda.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Hawa Mposi amelishukuru shirika hilo kwa msaada walioutoa na kusema kuwa kweli wamekuwa na nia ya dhati ya kusaidia kutatua tatizo hilo huku wakielewa kuwa hospitali hiyo bado haijaanza kutoa huduma.
Mposi amewaahidi wananchi wa Malinyi kuwa punde tu hospitali ikifunguliwa na huduma zikianza kutolewa wananchi watapata huduma bora tokana na walivyojipanga katika kutoa huduma bora za afya.
Naye mganga wa macho wa wilaya hiyo Stanford Mshomi amesema ifikapo Novemba 28 mwaka huu watafanya huduma ya upasuaji wa mtoto wa jicho katika hospitali hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.