Viongozi wilayani malinyi wametakiwa kuendele kuhamasisha jamii juu ya elimu ya afya na usafi wa mazingira hususani katika ujenzi na matumizi ya vyoo bora.
Kauli hiyo imetolewa na mgeni rasmi wakati akifungua warsha fupi ya kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira wilayani malinyi ndugu Lameck Lusesa ambaye pia ni katibu tawala wilayani hapo ambayo ilihusisha watendaji wa kata pamoja na viongozi mbalimbali kutoka halmashauri.
Katika warsha hiyo ambayo imebeba kauli mbiu isemayo USICHUKULIE POA NYUMBA NI CHOO Lusesa ameeleza kuwa wakazi walio wengi bado hawana uelewa wa kutosha juu ya ujenzi na matumizi ya vyoo vilivyo bora hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha tunatoka kwenye vyoo visivyoboreshwa na kuingia kwenye vyoo vilivyoboreshwa.
watendaji wa kata nao wakatoa changamoto mbalimbali zinazopelekea mpaka kuwepo na idadi kubwa ya kaya kutokuwa na vyoo ni pamoja na jamii kubwa ya wafugaji kwani wengi wao hawana vyoo au kuishi katika koo na kutumia choo kimoja, mwingiliano wa masuala ya kisiasa, uelewa mdogo wa elimu juu ya afya na usafi wa mazingira, , na hata kubomoka kwa vyoo vingi wakati wa masika.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.