Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Hawa Mposi amesema kati ya wanafunzi hao wavulana ni 460 na wasichana na 510 na shule 13 za sekondari ndizo zitatoa wanafunzi hao wilayani humo.
Mposi ameyasema hayo wakati wa semina kwa wasimamizi wa mtihani wa kidato cha nne iliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri mjini hapa.
Amesema maandalizi kwa sasa yapo vizuri hivyo kuwataka wasimamizi hao wawe wazalendo kwa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu na kusema kuwa wale wote watakaojihusisha na vitendo viovu serikali haitasita kuwachukulia hatua.
Mkurugenzi huyo mtendaji amewataka wasimamizi hao kuepuka takrima zinazoweza kusababisha usimamizi usio makini huku ikieleweka kuwa taifa limewaamini.
Amebainisha kuwa kama wakiingia katika udanganyifu katika usimamizi kunaweza sababisha kufutwa kwa mtihani au matokeo ya wanafunzi katika kituo husika ukizingatia kuwa maandalizi ya mitihani hiyo ni ya gharama kubwa.
Hata hivyo mkurugenzi huyo mtendaji amewatoa hofu wasimamizi hao kuwa wasiwe na wasiwasi kwani halmashauri imewaandalia stahiki zao na kilichobaki wao tu katika kutekeleza majukumu yao.
Aidha mkurugenzi huyo pia amewataka wakuu wa shule kuwa makini katika usimamizi na waandae mazingira rafiki ya ufanyaji kazi na kusiwepo na manung'uniko yoyote.
Kwa upande wao wasimamizi hao wamemuahidi mkurugenzi huyo mtendaji kuwa hawatamuangusha na watafanya kazi kwa umakini bila tamaa au uzembe wowote kama walivyokula viapo vyao.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.