Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla ametembelea Eneo la Hifadhi lenye Mgogoro Wilayani Malinyi. Eneo hilo ambalo ni Hifadhi limekuwa likilimwa na Wananchi kwa muda mrefu na kusababisha uharibifu mkubwa. Kwa Msimu huu wa Kilimo TANAPA wamezuia Wananchi hao kuendelea kulima na hivyo kupelekea mvutano mkubwa. Akihutubiana Wananchi wa Itete, Wilayani Malinyi Dk. Kingwangalla alisema yeye amekuja kuona uhalisia wa Mgogoro uliopo kati ya Wakulima na Hifadhi, hivyo ameliona tatizo na kwakuwa aliagizwa na Mh. Waziri Mkuu, yeye ataenda na kumwambia tatizo lilivyo na majibu yatatolewa baadae.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.