Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi leo tarehe 2/2/2019 limefanya kikao maalum cha kupitisha Rasimu ya mpango wa maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ya mwaka 2019/2020.
Katika Rasimu hiyo miradi mbalimbali inatarajiwa kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa stend ya abiria, ujenzi wa miundombinu ya dampo,ujenzi wa soko la wilaya, ujenzi wa bweni la wasichana sekondari ya usangule na ujenzi wa miundombinu ya mifugo ikiwemo mabirika, uzio wa minada. Pamoja na miradi hiyo halmashauri itaendelea kumalizia miradi viporo na pia kumalizia miradi iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi. Halmashauri ya wilaya inategemea kupata kiasi cha shilingi 19,535,254,274/= na kutumia Kiasi cha shilingi 19,355,952,910/= kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.