Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Malinyi limekaa kikao chake cha kawaida cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2017/2018. Kikao hicho kilipokea taarifa toka Kamati za Kudumu za Baraza la Madiwani, ambapo kila kamati iliwasilisha taarifa yake na wajumbe kupata muda wa kuijadili. Pamoja na kupokea taarifa hizo katika kikao hicho iliwasilishwa Rasimu ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019. Wajumbe waliupongeza Uongozi kwa kuandaa Rasimu nzuri yenye makisio ya Shilingi 2,200,000,000 (Bilioni mbili na laki mbili). Wajumbe walipendekeza kwa uongozi kuwa makini katika matumizi fedha zinazotengwa katika bajeti, waliweka msisitizo katika fedha zilizotengwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo, hii ni kutokana na Halmashauri kwa sasa kuwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta ya Afya na Elimu ambapo kila kijiji kipo katika hatua mbalimbali za ujenzi wa zahanati na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari kutokana ongezeko kubwa la uandikishaji wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza mwaka 2018. Pamoja na hayo Baraza lilitoa maazimio mbalimbali.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.