Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Malinyi limekaa kikao chake cha robo ya nne ya mwaka leo tarehe 1/09/2018 ikiwa ni kikao cha kufunga mwaka 2017/2018.Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ,ambapo kilihudhuriwa na mkurugenzi wa Halmashauri ,mkuu wa wilaya ,watumishi wa Halmashauri ,wadau mbalimbali wa vyama vya siasa na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi.
Katika kikao hicho madiwani wamejadili ajenda na Hoja mbalimbali za idara na vitengo ,ikiwemo idara ya fedha ,afya na Elimu, na kupitisha maazimio mbalimbali,vilevile kumekuwa na uchaguzi wa makamu mwenyekiti baada ya makamu aliyepita kumaliza muda wake,katika uchaguzi huo mheshimiwa Tira alipata nafasi ya kuwa makamu mwenyekiti kwa awamu nyingine tena, Pia mkurugenzi mpya Bwana Mussa Elias Mnyeti amesoma taarifa ya makabidhiano ya fedha na mali za Halmashauri kati yake na mkurugenzi aliyepita Bwana Mercelin Ndimbwa. Pia mkuu wa wilaya ambaye ni mualikwa aliwaomba madiwani ,mkurugenzi ,watumishi na wananchi kushirikiana ili kuleta maendeleo na ufanisi katika Halmashauri yetu ya wilaya ya Malinyi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.