Katibu Tawala wa Wilaya ya Malinyi Bwana Lameck Lusesa amezindua Baraza la Wafanyakazi katika Wilaya hii leo Tarehe 31 januari 2019, Baraza hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya wafanyakazi ,kutoka mkoani na wilaya ya ulanga.
Akizindua baraza hilo katibu tawala huyo amesisitiza kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha kati ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi ili kutatua matatizo ya wafanyakazi vilevile ameomba viongozi wa serikali pia watoe ushirikiano kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Bwana Lusesa pia ameomba viongozi wa vyama kuwasaidia wafanyakazi wa halmashauri wa Wilaya ya Malinyi kuunda vyama vya wafanyakazi kama Tughe na pia kupata miongozo na katiba.
Katika baraza hilo ulifanyika uchaguzi wa katibu wa baraza na katibu msaidizi,ambapo Ndg Christina Chacha amechaguliwa kuwa katibu wa baraza na Bwana Issa Matanda kuwa katibu msaidizi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.