Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba leo Machi 19, 2024 amezungumza na Wafanya biashara wa sukari katika maeneo ya Njiapanda ya songea, Mwenbeni , na Malinyi mjini juu ya maelekezo ya Serikali kuhusu bei elekezi ya sukari Wilayani Malinyi ambapo zoezi hilo pia limefanyika maeneo ya Mtimbira na Ngoheranga.
Mhe Waryuba amesema kutokana na changamoto ya sukari nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagiza sukari kuja Tanzania na kuisambaza maeneo mbalimblali ambapo Wilaya ya Malinyi ni miongoni mwa maeneo yaliyonufaika na sukatri hiyo na hivyo amewataka Wafanyabiashara Wilayani Malinyi kufuata maelekezo ya Serikali ya bei elekezi ya sukari isiyozidi shilingi elf tatu (3000) kwa kilo moja
"Mimi nawaambieni haya kama Kiongozi wenu, nawapeni tahadhari mapema, sukari iwe ya ruzuku ama isiyo ya ruzuku bei kwa kilo moja ni shilingi 3000,usipouza kwa bei hii iliyotangazwa na Serikali na ukauza kwa bei unayoijua wewe tutakukamata kwa kosa la kuhujumu uchumi" amesema Mhe. Waryuba
"Tunapokua na changamoto kama hii sio vyema Watanzania wengine wakatumia fursa hii kujinufaisha kwa kuweka bei kubwa ambayo inawaumiza Wananchi kwa kiasi kikubwa" amesema Mhe. Waryuba
Sambamba na hilo, Mkuu wa Wilaya Mhe. Sebastian Waryuba amewataka Wafanyabiashara Wilayani Malinyi kuzingatia uzalendo na Wafanyabiashara ambao walipata Sukari ya ruzuku na wakamaliza wasubiri utaratibu mwingine wa Serikali.
Hata hivyo, kufuatia zoezi hilo Mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Mohamed Salehe Ramadhan amekamatwa kwa kukiuka bei elekezi ya Serikali kwa kuuza sukari shilingi 3500 kwa kilo moja.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.