DC Waryuba ametoa mikakati hiyo alipokuwa akizungumza na Waalimu, Wakuu wa shule za Sekondari zote( Serikali na Binafsi) pamoja na Wadau wa elimu kwa ujumla katika kikao cha tathimini ya elimu sekondari kilichofanyika Februari 28, 2024 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Tumaini.
DC Waryuba amewapongeza Waalimu wa shule za Sekondari kwa kufaulisha kwa 75% ( kwa kidato cha pili na kidato cha nne) lakini amewataka Waalimu hao kutoridhika na matokeo hayo na badala yake watumie mikakati ya kisayansi ili kuongeza kiwango cha ufaulu na kutokomeza Ziro.
Aidha DC Waryuba ameitaka Ofisi ya Mkurugenzi kuunga mkono juhudi za Waalimu katika kuhakikisha mikakati ya kisayansi ya kutokomeza Ziro (sifuri) Wilayani Malinyi inafanikiwa kwa 100%
Sambamba na hilo Mhe. Sebastian Waryuba amemuagiza Mkuu wa Divisheni ya elimu Sekondari Bi Pendo Masalu kubaini Shule ambazo Wakuu wa shule hawana ubunifu na uwezo wa kusimamia taaluma na kuongeza kuwa kila Mkuu wa shule ahakikishe Waalimu wanamiliki ufaulishaji wa Wanafunzi.
Hata hivyo, baadhi ya Waalimu na Wadau wa elimu waliopata nafasi ya kuchangia maoni yao juu ya nini kifanyike ili kutokomeza Ziro, Waalimu hao pia wameweka bayana changamoto wanazokumbana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao,ikiwa ni pamoja na uqepo wa idadi kubwa ya Wanafunzi ukilinganisha na idadi ya Waalimu, kucheleweshwa/ kutokupata stahiki zao za msingi, mimba za utotoni pamoja na changamoto ya Lugha ya kingereza kwa Wanafunzi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.