Diwani wa Kata ya Usangule Mhe. Fadhili Nassoro Liguguda Januari 15, 2024 amefanya ziara katika shule ya Sekondari ya Usangule na kutoa vifaa vya michezo kwa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa shule hiyo ili kuleta hamasa ya michezo na kudhibiti utoro shuleni hapo.
Katika ziara hiyo Mhe. Diwani wa Kata ya Usangule aliambatana na Mtendaji wa Kata ya Usangule Bi Hellen George pamoja na Viongozi wa Baraza la maendeleo la Kata ya Usangule kufuatilia mwenendo wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza walioripoti shuleni hapo.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.