Oktoba 8, 2023
Hospitali ya Wilaya ya Malinyi kwa kushirikiana na Shirika la Solidar Med imezindua clinic tembezi ambayo itahudumia kata zote10 ikiwa na lengo la kufikia maeneo ambayo hayafikiki kirahisi kama vile Madabadaba, Ipera Asilia, Alabama, Kipenyo, Usangule, Kalengakero, Kiswago, Misegese, Mchangani, Kiwale, Lupunga, Ihowanja, na Kilosampepo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe.Sebastian Waryuba amelishukuru Shirika hilo kwa kuleta huduma hii na kuongeza kuwa huduma ya Clinic tembezi imekuja wakati muafaka kutokana na jiografia ya Wilaya ya Malinyi hasa nyakati za masika ambapo maeneo mengi hayafikiki kwa urahisi.
"Uwekezaji huu unaotembea wa thamani ya zaidi ya milioni 211 ni sehemu chache unaweza kuuona,Malinyi tumebahatika,Sasa tunakabidhi leo gari hili kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi,Wataalamu wa Afya wa Halmashauri itendeeni haki gari hii"amsema DC Waryuba
Aidha DC Waryuba ametoa Maelekezo kwa Ofisi ya Mkurugenzi kutengeneza mfumo rasmi wa kusimamia gari hilo usiokua na urasimu.
Kwaupande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Lucas Mgomahenga kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri amesema msaada huu wa Solidar Med unawaongezea Wananchi wa Malinyi unafuu wa kupata huduma za Afya na Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi itahakikisha gari hilo linafanya kazi iliyokusudiwa na Silidar Med.
Hapo awali, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Solidar Med Ndugu Benatus Sambili amesema kuwa Shirika hilo limefadhili utoaji wa gari hilo ambalo litatumika kama Clinic Tembezi lakini huduma zitakazotolewa zitafuata mfumo uleule wa Serkali.
"Anayepata huduma za Afya kwa kutumia Bima atapata huduma kwa mfumo huo huo,na anayepata huduma kwa kulipia atapata huduma kwa mfumo huohuo,na Watoa huduma ndani ya Clinic hii ni Wahudumu waliosajiliwa na kuajiriwa na Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi" Amesema Mkurugenzi huyo.
Akisoma Risala katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Clinic Tembezi Meneja Mradi Ndugu Frida Akyoo amesema huduma zitakazotolewa ni pamoja na Kufanya uchunguzi wa awali na matibabu kwa magonjwa yasiyoambukiza kama vile Kisukari na Shinikizo la damu, Kufanya uchunguzi wa awali na matibabu kwa magonjwa yanayoambukiza kama vile Kifua kikuu na VVU
Hata hivyo,Meneja huyo ameongeza kuwa Mradi huu unatarajia kuwafikia Walengwa kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja Jamii ya Wafugaji 5600, Watoto chini ya umri wa miaka mitano 8000,
Wakina Mama walio kwenye umri wa kujifungua 10,0000, Wakina Mama wanaonyonyesha 5000, Watu wenye Magonjwa sugu 2000, Watu waishio na VVU 62000, Wagonjwa wa Kifua kikuu 400 kwa mwaka,Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii 50, Wataalam wa Sekta ya Afya 50, na Timu ya uendeshaji huduma za Afya 20.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.