Agizo hilo limetolewa na waziri wa Tamisemi Ofisi ya Rais ,Mh. Seleman Jafo alipotembelea wilayani Malinyi hivi karibuni na kukagua ujenzi wa Hospital ya wilaya unaoendelea Wilayani hapa.
Waziri jafo alikagua majengo yote ya hospital na kisha kuongea na wananchi pamoja na mafundi wanaojenga hospital na kusikiliza kero zao na kuzitolea ufafanuzi kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya nahalmashauri pamoja na wataalamu ,alieleza kuwa ujenzi wa hospital hii ya wilaya umechelewa tofauti na muda uliopangwa kumaliza ujenzi huo, ambao umechelewa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mvua ambayo iliharibu miundombinu ya kufikisha vifaa kwa ajili ya ujenzi. Hivyo kutokana na changamoto hizo Waziri jafo aliongeza muda mpaka septemba 30 2019 majengo yote ya hospital yawe yamekamika .Aliwaasa wananchi kuacha tabia ya kufuata makundi ya wanasiasa ambao wanavuruga amani na yanarudisha nyuma maendeleo ya wilaya nzima ya Malinyi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.