Mratibu wa mradi wa TASAF Wilayani Malinyi Bi Sylivia Lussumo amesema Wilaya ya Malinyi inajivunia mradi wa TASAF kwa kuhudumia kaya 3253 ambayo ni sawa na vijiji 32 ambavyo vina jumla ya wanufaika 11739 kati yao Wanawake ni 6667 na Wanaume ni 5072.
Bi Sylivia amesema huduma zinazotolewa na mradi huo ni pamoja na ruzuku za kaya za walengwa wa TASAF, Kuwekeza akiba kupitia vikundi na miradi ya ajira za muda ambayo inafanyika katika vijiji 16 vya awali vilivyoanzishwa 2014.
Akielezea kuhusu malipo yanayotolewa kwa Wanufaika wa TASAF kuwa ni pamoja na malipo kwa walengwa ambao hawana nguvu kazi kuweza kufanya kazi, malipo ya ajira za muda, na malipo ya masharti ambayo yanajumuisha watoto wanaosoma na watoto wenye umri chini ya miaka 5.
Aidha Mratibu huyo ameongeza kuwa mzunguko huu wa awama ya 13 ambao ulianza tarehe 13/6 na kumalizika tarehe 15/6/2022 ulienda sambamba na zoezi la msingi la tathimini ya kaya katika vijiji 16 vya awali ili kujua maendeleo ya kaya hizi baada ya kuanza kupokea ruzuku kuanzia mwaka 2014.
Amefafanua kuwa afua zote zimekua za msingi sana na zimeweza kubadili na kuboresha mitazamo na maisha ya wanufaika wa mradi ambapo miongoni mwao wapo walioweza kujenga nyumba za kuishi, wengine wanajishughuliaha na ufugaji, kusomesha watoto, biashara ndogondogo, na kuwekeza kupitia vikundi ili kujipatia kipato kitakachokidhi mahitaji yao ya msingi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.