Septemba 26, 2023
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Gasto Silayo amekabidhi jumla ya vitabu 4559 vyenye thamani ya shilingi 20,746,242 vya masomo ya Sayansi (Mathematics na Biology) kwa Waalimu Wakuu wa Shule za Sekondari katika zoezi la kukabidhi vitabu hivyo lililofanyika katika Shule ya Msingi Nawigo.
Ndugu Silayo amewataka Waalimu kuhakikisha kuwa vitabu hivyo vinawafikia Wanafunzi Kama ilivyokusudiwa na Serikali na Wanafunzi wavitumie vitabu hivyo ipasavyo ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao na kufikia malengo yao .
"Sisi Kama Halmashauri tunajitahidi kuhakikisha kuwa tunapata Waalimu wa kutosha na wenye maadili ya kufanya kazi hiyo ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya kufundishia Kama vile madarasa na madawati ili Wanafunzi waweze kusoma vizuri na Waalimu waweze kufanya kazi zao vizuri" amesema Kaimu Mkurugenzi huyo.
Naye Afisa Elimu wa Wilaya Bi Pendo Masalu amewataka Waalimu kuwahimiza Wanafunzi kusoma vitabu, kufanya mazoezi yaliyo katika vitabu hivyo na na kuvitunza vitabu hivyo ili Wanafunzi wengingine watapokuja wavikute vitabu hivyo vikiwa katika hali nzuri.
Akisoma idadi ya vitabu vilivyokabidhiwa Bi Pendo Masalu amesema kwa somo la hesabu (Mathematics) kidato cha kwanza ni vitabu 425, Kidato cha pili vitabu 644,
Kidato cha tatu vitabu 553, na Kidato cha nne ni vitabu 753, Kwa upande wa somo la Biolojia (Biology) kidato cha kwanza ni vitabu 514, kidato cha pili vitabu 578, kidato cha tatu vitabu 378 na Kidato cha nne vitabu 714.
"Ninaishuku Serikali kwa kutuletea vitabu hivi, ninaamini vitaziba pengo lililokuwepo kwani Shule zote zilikua na uhaba wa vitabu, kwa masomo haya tiliyopata vitabu hatutakiwi kufeli, lakini tunaiomba Serikali ituletee vitabu vya masomo yaliyobakia (Physics na Chemistry)" amesema Afisa Elimu Wilaya .
Hata hivyo, baadhi ya Waalimu Wakuu waliopokea vitabu hivyo wamesema wanamshukuru Mhe. Rais wa awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona kwamba Waalimu wanaweza kufanya kazi vizuri zaidi wakiwa na vitabu kwasababu Waalimu wanapata changamoto sana kufundisha Wanafunzi kwasababu ya uhaba wa vitabu, hivyo basi vitabu hivyo vitawasaidia Wanafunzi kupata uelewa na kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.