Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi Bwana Absalom Gepson amefungua kikao cha kutathimini upimaji wa kusoma na kuandika(KK) katika shule za Msingi za halmashauri ya wilaya ya Malinyi kwa darasa la pili ,leo hii tarehe 28/03/2018 kilichofanyika katika shule ya msingi Nawigo.Washiriki wa kikao hicho ni Afisa Elimu msingi wilaya ya Malinyi, na maafisa wengine wa elimu wilayani, Maafisa Elimu kata zote pamoja na wadau wa mpango wa Tusome Pamoja.
Tathimini hiyo ilifanyika kutokana na matokeo ya zoezi la upimaji lililofanyika kwa mfumo wa DPLA(Decentralized Periodic Learning Assessment) ngazi ya shule za msingi kwa darasa la pili kwa awamu mbili ambayo ni mwezi Aprili na mwezi oktoba 2017. Upimaji huo ulihusu viwango vya utendaji wa shule na stadi ya kusoma na kuandika.
Tathimini inaonyesha shule za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi zimeshinda kwa vigezo 8 kati ya 14 vilivyotumika katika upimaji.Kufuatia tathimini hiyo hiyo Afisa Elimu Msingi Bwana S.Kalagila amewaagiza maafisa elimu kata hao kusimamia utekelezaji wa mitaala katika shule zao ili kuhakikisha wanafunzi wanapata Elimu stahiki na Walimu wanatimiza wajibu wao.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.