Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Wilaya ya ilifanya ziara ya Mafunzo katika Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa mnamo tarehe 20/02/2018. Lengo la ziara hiyo ilikuwa kwenda kujionea jengo la Halmashauri ya Kilolo kutokana na Halmashauri ya Malinyi kuwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri. Mchoro wa jengo la Halamashauri ya wilaya ya Malinyi umechukuliwa toka Halmashauri ya Kilolo hivyo wajumbe hao waliona ni vyema kwenda kuona muonekano halisi wa jengo hilo. Hakika wajumbe wa kamati hiyo walifurahia kuona jengo hilo lililokuwa na kila aina ya sifa, yaani muonekano wake kwa nje na mgawanyo wa ofisi mbalimbali ndani ya jengo. Pamoja na kuona jengo hilo pia kamati ilipata kujifunza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali. Aidha kamati ilivutiwa sana na utekelezaji wa mmradi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya ambao majengo yake yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi. Akielezea mafanikio ya halmashauri ya wilaya ya Kilolo, Mkurugenzi wa wilaya hiyo bwana Kweze alisema, siri kubwa ya mafanikio hayo ni ushirikiano uliopo baina ya watendaji wakuu wa halmashauri yaani Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi na Wakuu wa Idara. Kwa mfano alisema kuwa miradi yao mingi imepatikana kutokana na maandiko (Proposal) ambapo baada ya kukamika kwa andiko/maandiko huwa wanatoka kwa umoja wao na kwenda kwa wahisani mbalimbali kama vile ofisi za mabalozi, mashirika ya kimataifa, NGOs n.k. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi Bw. Marcelin Ndimbwa aliwasifu watendaji wa halamashauri ya Kilolo kuanzia Mwenyekiti wa Halmashauri, Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara kwa utendaji kazi wao hadi kupelekea wilaya ya Kilolo pamoja na uchanga wake kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi Bw. Fadhili Liguguda wakati alipotoa neno na shukrani alikiri kuwa safari yao ilikuwa ni yenye manufaa mno, kwani wamejifunza mengi hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Pia Mwenyekiti huyo aliwawakaribisha Waheshimiwa Madiwani hasa Kamati ya fedha na Mipango watembelee Halmashauri ya wilaya ya Malinyi kwani kuna mambo wanmaweza kujifunza, mualiko huo ulikubaliwa kwa mikono miwili kwani Mwenyekiti wa Hamashauri ya Wilaya ya Kilolo kwa niaba ya halmashauri alisema wamekubali kutembelea Malinyi kabla ya mwezi Mei.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.