Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bwana Musa Mnyeti ameshiriki katika utambulisho wa kamati ya Lishe Endelevu ya Halmashauri ya Wilaya tarehe 21/03/2019.
Mradi huu wa Lishe Endelevu unafadhiliwa na US AID –MAREKANI,mradi utaendeshwa kwa muda wa miaka mine 2018-2021,ambapo utashughulika na kuwahudumia watoto wa chini ya miaka mitano ,wasichana kuanzia miaka 15-19 pamoja na wanawake miaka 15-49 wenye umri wa kuzaa. Mradi huu unaendeshwa katika mikoa minne ambayo ni Morogoro, Dodoma, RUkwa na Iringa.
Lengo la mradi ni kuwasaidia wananchi kuelewa elimu ya lishe na kutumia lishe kwa ajili ya ukuaji wa watoto,kuondoa udumavu wa akili na mwili,elimu ya unyonyeshaji na lishe ya ziada katika makuzi ya siku 1000 za mtoto na kupunguza utapiamlo wa chini na wa juu.
Katika utambulisho huu kamati ilielekezwa majukumu yake katika halmashauri ambapo ni pamoja na kusimamia shughuli zote za lishe .
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.