Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ni miongoni mwa Halmashauri 9 zilizopo Mkoani Morogoro ambazo zimewasilisha taarifa zao za kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya 6 katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Mkuu wa Mkoa, Msemaji Mkuu wa Serikali na Wakurugenzi wa Halmaashauri.
Akitoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita kwa niaba ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mkurugenzi Mtendaji ndugu Rehema Said Bwasi amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu Serikali ya awamu ya sita imewasikia na imewafikia Wananchi wa Wilaya ya Malinyi katika sekta ya afya kwa kuwapatia fedha kiasi cha shilingi 1,490,000,000 amabazo zimefanikisha ujenzi wa miundombinu ya afya kwa kujenga Zahanati 7, Kituo cha afya 1 , Wodi 3 katika Hospitali ya wilaya, Jengo la wagonjwa wa dharura(Emergency) na nyumba 4 za watumishi.
Mkurugenzi Mtendaji ameongeza kuwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa fedha shilingi 1,650,000,000/= kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya. hali ambayo imerahisisha upatikanaji wa huduma za afya ambapo hapo awali wananchi walikuwa wanalazimika kwenda Ifakara umbali wa kilomita 150 au Morogoro umbali wa km 380 kufuata huduma za afya, lakini kwa sasa Wananchi wa Wilaya ya Malinyi wanfurahia huduma mbalimbali kama vile upasuaji mkubwa, huduma za kulaza wagunjwa, huduma za Mama na Mtoto, X- ray, na sonography kutoka katika Hospitali ya wilayan yenye madaktari na wauguzi wabobezi na vifaa vya kisasa
Sambamba na hilo, Serikali ya awamu ya sita imewasikia na imewafika Wananchi wa Wilaya ya Malinyi katika sekta ya elimu msingi ambapo jumla ya shilingi 3,357,000,000/= zimtolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu, na hivyo kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 157, matundu ya vyoo 220 , nyumba za walimu 7 na shule Mpya za Msingi 2.
Mhe. Rais pia ametoa jumla ya shilingi 1,217,127,501.24 kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa elimu kupitia será ya serikali ya elimu bila malipo. Haya yote yameleta manufaa makubwa kwa wananchi kwani mazingira sasa ya kujifunzia yameboreka, umbali wa kuitafuta elimu umepungua hivyo uandikishaji wa wanafunzi umeongezeka na utoro wa rejareja umepungua.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hakuishia hapo lakini pia amewasikia na kuwafikia Wananchi wa Malinyi katika sekta ya elimu Sekondari ambapo jumla ya shilingi 1,633,347,000/= zimetumika kujenga vyumba vya madarasa 63, vyumba vya maabara 17, mabweni 3, na nyumba za walimu 2. katika kipindi cha serika ya awamu ya sita pia umefanyika ujenzi wa shule mbili mpya za Sekondari kupitia mradi wa SEQUIP ambao umegharimu jumla ya shilingi 998,000,000/=
Kuhusu uwezeshaji kiuchumi jumla ya vikundi 156 ndani ya wilaya hii vimekopeshwa fedha Tshs. 1,112,825,749/= za 10% ya mapato ya ndani, Kati ya vikundi hivyo, 82 ni vya wanawake, 40 vya Vijana na 12 vya watu wenye ulemavu.
Pamoja na hayo, Serikali ya awamunya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imwafikia Wananchi wa Malinyi katika sekta ya maji kupitia Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA, Kuboresha miundombinu ya barabara kupitia Wakala wa barabara za mijini na Vijijini TARUURA, na kuhakikisha huduma ya nishati ya umeme inapatikana Wilayani Malinyi kupitia Mradi wa REA.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.