Wazazi na walimu wa shule ya msingi Nawigo wametakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha mazingira mazuri ya taaluma kwa watoto wao.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Rashid Kiding’a wakati wa kikao cha walimu na wazazi kilichofanyika shuleni hapo huku kikiwa na lengo la kukuza taaluma.
Kinding’a ameeleza kuwa wazazi wamekuwa wakiwaacha watoto na kuhamia shamba hali inayopelekea watoto kuwa wenyewe bila mwangalizi wa karibu hivyo ni vyema kuangalia suala la elimu kwa jicho la pili ili kufanikisha maendeleo ya mtoto.
Nae mwalimu mkuu wa shule hiyo Henry Njelekele ameongeza kuwa suala la kumwandaa mtoto na kujifunza ili kufanikisha anapata kile anachostahili ni jukumu lao kwa pamoja hivyo wahakikishe wanatambua wajibu wao kwa mwanafunzi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.