katika kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani watumishi wa halmashauri ya wilaya ya malinyi wameadhimisha siku hiyo kwa kwenda kuwaona wagonjwa katika hospiatali ya kilutheri LUGALA.
Hata hivyo mara baada ya kutoka hospitali maandamano yalianza moja kwa moja mpaka katika viwanja vya shule ya msingi Nawigo ambapo kuliandaliwa mambo mbalimbali ili kuweza kusherehesha sherehe hizo ambapo mgeni rasmi akiwa katibu tawala wilaya bwana Lameck Lusesa.
Aidha katika hotuba yake Lusesa amesema kuwa watumishi wote wanatakiwa kujenga mshikamano mzuri baina ya wao kwa wao pamoja na viongozi wao kwani kwa kufanya hivyo hupelekea kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko kukawa hakuna maelewano yaliyo mazuri.
kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGWU Thadeus Macha ametoa rai kwa wafanyakazi ambao bado mpaka sasa hawajajiunga katika vyama mbalimbali vya wafanyakazi kujiunga mapema kwani vyama hivyo ni ngome kwao.
maadhimisho ya siku ya wafanyakazi huadhimishwa mei mosi kila mwaka duniani kote na kauli mbiu ya mwaka huu ni UCHUMI WA VIWANDA UZINGATIWE HAKI MASLAHI NA HESHIMA KWA WAFANYAKAZI ambapo nchini tanzania imeungana na nchi zingine duniani kote kuadhimisha siku hii ambapo kitaifa imefanyika katika viwanja vya ushirika wilayani moshi mkoani Kilimanjaro huku mgeni rasmi akiwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania DK John Pombe Magufuli.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.