Julai 25, 2023
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Ndugu Absalom Gepson leo Julai 25, 2023 wameungana na Watanzania wengine nchini kuadhimisha siku ya mashujaa kwa kufanya Usafi wa Mazingira katika eneo la stendi mpya lililopo Misegese Wilayani Malinyi.
"Sasa hivi hatupigani, nchi yetu Ina amani, hatuhitaji kupoteza nguvu kwenye masuala mengine, tunatumia nguvu kwenye masuala ya kuinua uchumi wa Taifa kwa kufanya kazi kwa bidii" Amesema Kaimu Mkurugenzi Ndugu Absalom Gepson.
Aidha Ndugu Absalom amewashukuru Wakuu wa Idara na Watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwa kushiriki katika kusafisha mazingira yanayozunguka eneo hilo la Stendi mpya inayotarajiwa kuanzia kufanya kazi mwezi ujao.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.