Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ambao pia ni Wajumbe wa Kamati ya Mipango na Fedha Agost 14, 2023 wametembelea miradi ya Boost kujionea maendeleo ya miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Shule ya Msingi Mwembeni ambayo ilipokea shilingi milioni 570,300,000 kwaajili ya ujenzi wa Shule Mpya yenye mikondo miwili, ikijumuisha madarasa14,, vyoo matundu 16, jengo la utawala, darasa la awali nyumba ya Mtumishi, na Kichomea taka
Shule ya Msingi Njiwa ilipokea shilingi milioni 306,900,000 kwaajili ya ujenzi wa Shule yenye mkondo mmoja, ikijumuisha madarasa 7,madarasa ya awali 2, jengo la utawala, vyoo matundu 8,na Kichomea taka.
Akiongea wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mhe Pius Mwelase amewataka Waalimu Wakuu wa Shule hizo kuharakisha kasi ya ujenzi wa mdarasa hayo ili yaweze kutumika kwani ujenzi huo uko nyuma ya wakati kutokana na kuchelewa kuanza kwa utekelezaji wa Miradi hiyo .
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.