Watumishi wa umma wilayani malinyi wametakiwa kuzingatia na kuyafanyia kazi mafunzo yanayotolewa na mashirika mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa na mgeni rasmi Richard Likalangu ambaye alimwakilisha mwenyekiti wa halmashuri katika mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Likalangu amesema kuwa mafunzo yanayotolewa ni vyema yakazingatiwa na kutekelezwa popote wanapokuwa na si kuachana nayo pasipo kufanyia kazi kwani imeonekana kuwa ni kasumba kubwa kwa watumishi waliowengi.
Hata hivyo amewataka kufahamu umuhimu wa maadili ikiwemo kujenga imani ya wananchi kwa serikali yao na taasisi za umma, kujenga dhana ya uzalendo, utaifa , nidhamu utu utendaji na ufanisi wa kazi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.