Kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa tarehe 12 kwenda 13, mvua hiyo imesababisha mafuriko ya maji katika mto Furuwa. Mafuriko hayo yamesababisha kufungwa kwa baadhi ya barabara wilayani Malinyi, nyumba kadhaa zimebomolewa na familia nyingi kukosa mahali pa kuishi. Akizungumza na wananchi eneo la njia panda ya Songea Mkuu wa wilaya ya Malinyi Ndg. Majura Kasika alisema kuwa ametembelea maeneo mbalimbali ya wilaya kuanzia Malinyi mjini, Lugala na Misegese kujionea hali halisi na uhalibifu uliojitokeza ili akae na kamati yake ya maafa ili watoe taarifa mkoani kwa msaada zaidi. Aidha amewapa pole wale wote waliopata maafa kutokana na mafuriko hayo. Pia amewaasa wananchi wa Malinyi kutunza vyema kingo za mto Furuwa kwani kuna uharibifu mkubwa pembezoni mwa mto huo jambo linalopelekea maji kumwagika nje ya kingo kwa urahisi. Habari zaidi ya matukio mbalimbali ya mafuriko hayo itatolewa baada ya tathmini ya athari itakapotolewa na kamati ya maafa.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.