Halmashauri ya Malinyi imedhamilia kwa dhati kuongeza upatikanaji wa Chakula Mashuleni, hilo limeongelewa leo tarehe 16.10.2020 kwenye kikao cha Lishe kilichofanyika Makao Mapya ya Halmashauri eneo la Misegese na Mwenyekiti wa Kikao Ndg. MARTIN MUHODE.
Katika kikao hicho cha Lishe, kwa pamoja wajumbe waliazimia kuunda kamati ndogo itakayofuatilia jinsi gani Walimu, Wanafunzi na Kamati za Shule watakavyoweza kushirikiana ili kuhakikisha Shule zinakuwa na Mashamba ambayo yatazalisha Chakula kwaajili ya Wanafunzi.
Pia Kikao kilielekeza Shule ziwe na Mashamba ya Matunda pamoja na Bustani za Mboga za Majani ili kupata matunda na Mboga za Majani kwaajili ya Wanafunzi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.