Halmashauri ya wilaya ya malinyi imefanya mnada wa kwanza wa zao la ufuta kwa wakulima kupitia mfumo wa stakabadhi
ghalani ambao umeazimiwa na halmashauri hiyo kutumika katika msimu huu wa mavuno. katika mnada huo wa kwanza chama
kikuu cha ushirika UKICU kimeuza kilogramu 12,400 za ufuta kwa mnada ambao umeshirikisha wakulima wa zao hilo kupitia
vyama vya msingi vya wakulima AMCOS.
katika mnada huo vyama vya msingi vilivyouza ufuta katika mnada huo ni malinyi ambao wameuza kilogramu 7,950 ,Igaluki
waliuza kilogramu 3,950 na mkombozi wameuza kilogramu 500.
kupitia mnada huo kampuni ya Afrissian Ginning LTD wameshinda mnada huo kwa kununua ufuta kwa bei ya shilingi 3,400/
kwa kilo.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.