Mkuu wa Wilaya ya Malinyi bwana Majula Kasika amezindua mchakato wa uanzishaji wa Baraza la biashara la Wilaya ya malinyi , uzinduzi huo umefanyika katika ukumbu wa Halmashauri ya wilaya mwanzoni mwa wiki hii . Baraza la biashara linaundwa na pande mbili ambazo ni upande wa Serikali na Sector binafsi. Akiongea katika uzinduzi huo mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa kuundwa kwa baraza la Biashara wilayani ni suluhu kwa wafanyabiashara, wakulima na wafugaji, pia amewataka wananchi na wafanyabiashara kuhamasishana ili kuunda baraza lenye nguvu ambalo litaweza kuwasaidia katika maendeleo ya biashara , kilimo na ufugaji,. Katika uzinduzi huo kamati ya watu watano toka sekta binafsi iliundwa ili kusimamia mchakato wa kuunda Baraza la Biashara.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.