Jumla ya shilingi milioni 128 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri zitatutumika kumalizia ujenzi wa jengo la dharura, jengo la nyumba ya Watumishi (3 in 1) jengo la Utawala na jengo la Wazazi.
Hayo yamesemwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Dkt. Joseph Masolwa wakati akisoma taarifa juu ya mwenendo wa ujenzi na umaliziaji wa majengo hayo kwa kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ilipofanya ziara ya kukagua miradi katika Hospitali ya Wilaya ya Malinyi.
Dkt. Masolwa amefafanua kuwa mwezi wa nane (August 2023) Hospitali ya Wilaya ilpokea kiasi cha shilingi milioni 82 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo milioni 60 zililenga kumalizia ujenzi wa jengo la dharura, milioni 22 zililenga kumalizia ujenzi wa nyumba ya Watumishi ( 3 in 1) na mwishoni mwa mwezi wa kumi (Oktoba 2023) Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi milioni 46 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo milioni 30 zimelenga kumalizia ujenzi wa jengo la Wazazi na milioni 16 zitamalizia ujenzi wa jengo la utawala.
Naye Mhandisi wa Wa Wilaya Ndugu Fokward Mhoisol amesema kuwa kwa sasa shughuli za umaliziaji wa majengo hayo zimekwishaanza na majengo hayo yapo katika hatua mbalimbali za umaliziaji ambapo jengo la utawala limekamilika kwa 71%, jengo la dharura limekamilika kwa 95%, nyumba ya Watumishi kwa 92% jengonla Wazazi limekamilika na linaendelea kutoa huduma.
Aidha Mhandisi Fokward ameongeza kuwa kwa mujibu wa mpango kazi wa Idara ya ujenzi mpaka kufikia tarehe 30/10 /2023 jengo la dharura, nyumba ya Watumishi itakua imekamilika, ambapo jengo la Utawala linatarajiwa kukamilika tarehe 15/11/2023.
Hata hivyo, Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imeipongeza Idara ya ujenzi kwa hatua iliyofikia katika usimamizi wa ujenzi wa majengo hayo na kuitaka iendelee kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja kuongeza umakini katika kusimamia matumizi ya fedha za Serikali na kusimamia mafundi ili miradi hiyo ikamilike ndani ya muda uliokusudiwa.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.