Mkuu wa mkoa wa Morogoro dr Kebwe Steven Kebwe leo ameungana na wanamalinyi kufanya usafi ikiwa ni agizo la rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania dkt John Pombe Magufuli kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Zoezi hilo la usafi ambalo limefanyika katika maeneo ya soko la bidhaa mbalimbali malinyi mjini limehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa halmashauri pamoja na wananchi kwa ujumla.
Hata hivyo wakazi wa malinyi wamefurahishwa na kitendo kilichofanywa na mkuu wa mkoa kushirikinao kwani wameona kama ni bahati kwa kiongozi mkubwa wa mkoa kufanya hivyo tena kwa wilaya ambayo ni mpya.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.