Mkuu wa MKoa Mhe.Adam Kighoma Malima amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi pamoja na kuongoza kikao cha kufanya tathmini za hoja za Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali.
Miradi hiyo iliyotembelewa tarehe 5-6 mwezi wa 6 ni pamoja na Kituo cha afya Itete, Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Kituo cha afya Ngoheranga, Kivuko cha Kikove, na Hospitali ya Wilaya ya Malinyi.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Malinyi, Mkuu wa Mkoa alitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya na watendaji wake kuhusu bei elekezi ya mnada (Stakabadhi ghalani)kwa zao la ufuta kuwa ni shilingi 3400 na yeyote atakayepotosha mfumo huu wa Serikali hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha, Mkuu wa Mkoa Mhe.Adam Kighoma Malima aliielekeza Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)kuhakikisha wakazi wa kijiji cha Malinyi wanapata huduma ya maji safi na salama ndani ya siku mbili tarehe( 5-6) kupitia vyanzo vya Maji vya Mradi huo kwa kuwa Mradi huo umeshakamilika.
Mkuu wa Mkoa pia amewataka wakazi wa kijiji cha Itete kumiliki idadi ya mifugo wanayoweza kuihudumia ili isilete uharibifu wa mazao katika mashamba ya Wakulima na kuharibu vyanzo vya maji.
Akitolea ufafanuzi kuhusu maeneo korofi ya miundombinu ya barabara ya Malinyi, Mhe.Adam Kighoma Malima amesema atashirikiana na Meneja wa TANROAD Mkoa, pamoja na Injinia wa Mkoa kutafuta ufumbuzi wa haraka ili Wananchi wasiendelee kuumia, Wanunuzi wa mazao wasiendelee kuwaminya Wakulima kwa kigezo cha barabara na kurahisisha mawasiliano kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi na Ulanga.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.