Mhe. Sebastian Waryuba Julai 28, 2023 amekabidhi mpira wa miguu, mpira wa Pete, jezi, na magoli 2 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Daniel Godfrey Chongolo tarehe 1/2/2023 alipotembelea shuleni hapo pamoja na Viongozi wengine .
Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa lengo la Serikali ni kuona watoto wanasoma kwa bidii ili watimize malengo yao, lakini Elimu inaendana na michezo kwa kua michezo huimarisha akili.
Mhe. Sebastian Waryuba akatoa wito kwa Walimu kuhimiza michezo shuleni kwakua michezo Ina faida kubwa sana na kuongeza kuwa michezo ni ajira.
"Nisingeweza kuja hivihivi na mikono mitupu, nikaona nije na mikono iliyonyooka, nilitanguliza magoli, na leo nimekuja na vifaa vingine vya michezo" amesema Mhe. Sebastian Waryuba.
Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Njiwa Ndugu Issa Said Matekula akawataka Wazazi kuonyesha uzalendo kwa watoto na kuwalea katika maadili yanayotakikana katika maendeleo ya shule na jamii kwa ujumla.
Ghafla hiyo ya kukabidhi vifaa vya michezo ilihudhuriwa na Afisa Elimu Sekondari Wilaya kwa niaba ya Mkurugenzi, Waalimu wa Shule ya Sekondari Njiwa, Viongozi wa Chama na Serikali Kata ya Njiwa,Viongozi wa dini na Maafisa mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi.
Mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kukabidhi vifaa hivyo vya michezo, Mkuu wa Wilaya alishiriki chakula cha mchana pamoja na Wanafunzi wa Shule hiyo ili kuhakikisha kuwa Elimu na mahusiano yanasonga mbele.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.