Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi Rehema Bwasi Leo Julai 24, 2023 ameungana na Wakulima na Wananchi kwa ujumla kushuhudia mnada wa 5 wa zao la ufuta kwa mfumo wa Stakabadhi Ghalani ambapo jumla kg 223,560 zimeuzwa kwa bei ya shilingi 3540 kwa kilo Moja.
Bi Rehema Bwasi amesema kuwa kwa msimu ujao Halmashauri inajipanga kuimarisha vyama vya msingi katika Kila Kijiji ili viweze kisimama kwa maslahi ya Wakulima na kuviunganisha vyama hivyo na Taasisi za fedha ili Wakulima waweze kupata mikopo itakayowawezesha kununua pembejeo za kilimo.
"SASA TUNAIMBA WIMBO MMOJA WA SHANGWE"
"MAMBO YOTE SASA NI STAKABADHI GHALANI"
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.