UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU
Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini hali ya miundombinu ya barabara kwa baadhi ya maeneo wilayani malinyi imezidi kuwa ni changamoto.
Hata hivyo vyombo vya usafiri vinalazimika kutumia barabara za mitaa kutoka standi ya mabasi mpaka barabara kubwa kutokana na kuharibika.
Aidha hata barabara hizo za mitaa zinazotumika zinaoonekana kuwa bado ni tatizo kwani nazo zimeharibiwa na mvua na kusababisha magari kukwama.
Idara ya ujenzi imetembelea maeneo hayo na kutona tatizo na yayari kazi imekwisha anza kukarabati maeneo hayo.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.