Hivi karibuni kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu 2019 bwana Mzee Ally Mkongea ameongoza wakimbiza mwenge Kufungua,kuzindua na kuangalia miradi mbalimbali ya maendeleo yenye jumla ya thamani ya shilingi 12,442,171,000.Gharama za uchangiaji wa miradi hiyo ni nguvu za wananchi shilingi 181,080,000.,halmashauri shilingi million tano, serikali kuu ni shs 815,739,000 na wahisani ni shilingi 11,000,352,000.katika miradi hiyo mmoja umeonwa,mmoja umewekea jiwe la msingi,mmoja wa kuzinduliwa nakufunguliwa,miradi hiyo ni ujenzi na ukarabati chuo cha maendeleo ya wananchi sofi, uchimbaji na ujenzi wa visima virefu,mradi wa uzalishaji miche, ufugaji wa nyuki na kuhifadhi mazingira na mradi wa urasimishaji ardhi Wilayani Malinyi.
Baada ya kupitia miradi hiyo mwenge wa uhuru ulielekea kwenye viwanja vya mkesha tarafa ya Ngoheranga kwenye viwanja vya kituo cha Afya Ngoheranga ,ambapo Risala ya utii kwa MH. Rais ilisomwa na viongozi wa wilaya,kamati ya ulinzi na usalama na watumishi wote wa serikali wilayani Malinyi,baadaye kiongozi huyo kitaifa alitoa ujumbe wa mwenge wa mwaka 2019 kwa wananchi ambapo ujumbe wa mwaka huu ni utunzaji wa vyanzo vya maji,kutokomeza malaria ,vita dhidi ya rushwa na dawa za kulevya,upimaji wa VVU.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.