Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani, leo tarehe 16 Julai 2017 kwa mara ya kwanza amekwenda Songea kupitia Barabara ya Ruaha-Ifakara-Lupilo-Malinyi-Londo-Lumecha/Songea.
Barabara hiyo ambayo ni kilio cha muda mrefu kwa wananchi waishio Malinyi na Songea sasa imefunguka rasmi. Akiongea na wananchi wa kijiji cha Ihowanja Wilayani Malinyi, Muhandisi Ngonyani ameipongeza Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kutimiza ahadi yake ya kuitengeneza Barabara hiyo ambayo iliinadi wakati wa kampeni.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani, amesema kuwa ameamua kupita mwenyewe kwenye barabara hiyo ili kujionea changamoto zilizobaki ili serikali izitatue na hatimaye hata Gari za kawaida ziweze kupita.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.