Kauli hiyo imetolewa na kaimu mkuu wa wilaya ya Malinyi Mhe.Ngollo Ng’waniduhu Malenya kwenye uzinduzi wa upimaji wa afya ,ambao umefanyika tarehe 05/11/2018 wilayani hapa katika viwanja vya Toboa. Katika uzinduzi huo huduma mbalimbali zilitolewa kama uchangiaji damu, upimaji wa virusi vya ukimwi,upimaji wa shinikizo la damu, kisukari na Tohara kwa wanaume. Akiongea na wananchi wa Malinyi kaimu huyo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ulanga , amewaasa wazazi kuwa kioo kwa familia ili watoto wao wakue katika maadili mema, vilevile wazazi wanapaswa kuwalinda watoto wa kike,na pia amewaonya wasichana kuepuka kurubuniwa na wanaume,pia amepiga marafuku ngoma zote zinazohamasisha ngono zembe badala yake wacheze ngoma zinazotoa mafunzo na maonyo kwa jamii.
Mkuu huyo pia amewaagiza vijana wa kiume wajishughulishe na shughuli halali zinazoweza kuwapatia kipato . vilevile amewasihi wanaume kujali afya zao kwa kupima afya zao.
Kauli mbiu ya uzinduzi huu ni “Furaha yangu, mimi nipo Tayari kulinda Afya yangu Wewe je?”
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.