PROGRAMU ya uchefuaji inayoendeshwa na idara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Health Actions Promotion Association(HAPA) wilayani Malinyi imeleta mafanikio baada ya kaya nyingi kuamua kuacha kujisaidia maporini na kujenga vyoo bora.Akizindua zoezi la uhamasishaji wa usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora katika katika ya Malinyi tarehe 23 novemba 2018,MKUU Wa Wilaya hiyo Majura Kasika amesema zoezi hilo liendelee kwa vijiji vyote na itakapofika Disemba 30 mwaka huu kila kaya katika wilaya hiyo lazima iwe na choo bora.Kasika amesema wataalamu wa afya kwa kushirikiana na wadau Wa usafi Wa mazingira kuendelea na zoezi la kuwawekea pembeni vinyesi wakati Wa kula kaya zote zisizokuwa na vyoo ili Jamii hizo kuchefuka na hatimae kujenga vyoo bora ili kuepukana na magonjwa ya milipuko.
Kasika alisema ni aibu kwa Wilaya ya Malinyi wananchi wake kuendelea kukosa vyoo ukizingatia kuwa muda mfupi ujao mvua za masika zitaanza kunyesha na maeneo mengi kuwa na Maji hivyo magonjwa ya milipuko yataibuka kila sehemu pasipochukuliwa hatua za haraka,Ameitaka sekta ya Afya kwa kushirikiana na viongozi Wa vijiji kutumia Sheria zao ndogo walizojiwekea kwa kupiga faini wale wasiokuwa na vyoo na kuendelea na programu ya uchefuaji ili kila mkoja aone umuhimu wa kuwa na choo.Amesema zoezi linaloendeshwa na taasisi ya HAPA limekuwa na mafanikio makubwa katika Wilaya kwani toka waanze shughuli wilayani humo wamehamasisha vya kutosha kutoka kaya 8,094 hadi kufikia kaya 5369 hivyo juhudi zaidi zinahitajika ili kaya hizo zishuke hadi kufikia kaya 1000.
Amebainisha kuwa Wilaya ya Malinyi ina wakazi wengi Wa Jamii ya kifugaji ambao ndio hawana vyoo na kusema kuwa programu ya uchefuaji ndio imekuwa na mafanikio ya ujenzi Wa vyoo na ana imani hadi ifikapo Desemba 30 mwaka huu Wilaya itatekeleza kwa kiasi kikubwa agizo la Makamu Wa Rais la kila kaya iwe na choo bora kinachotumika.Awali akisoma taarifa ya uhamasishaji Wa usafi Wa mazingira na ujenzi Wa vyoo bora,Meneja Wa HAPA Malinyi Focus Mtaki alisema kwa kushirikiana na halmashauri hadi kufikia Septemba mwaka huu wamefanya tathmini ya hali ya vyoo katika kaya ndani ya vijiji 33 wilayani humo.
Mtaki amesema katika tathmini hiyo takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya kaya zote zilizotembelewa ni 22425 na idadi ya kaya zenye vyoo ni 17056 Sawa na asilimia 76 na kaya hazina vyoo ni 5369 huku kaya zenye kifaa cha kunawia mikono ni 3082.Hata hivyo Meneja huyo Wa HAPA amesema ili kufikia malengo ya kitaifa wao na Wilaya wamejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo kwa kaya ambazo hazina vyoo 5369 matumizi ya Sheria ndogo zitumike ili kuhakikisha zinajenga na kutumia vyoo bora kufikia Disemba 2018 na kaya zenye vyoo vya asili ambazo ni 12986 kuboresha vyoo.Mikakati mingine ni wananchi kuhimizwa kuweka vifaa vya kunawia mikono Mara baada ya kutoka chooni,viongozi Wa kata,vijiji hadi vitongoji kujenga na kuboresha vyoo vyao na viongozi Wa dini,siasa na Asasi za kiraia wahimize ujenzi na matumizi ya vyoo bora na unawaji mikono kwa Maji na Sabuni baada ya kutoka chooni.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.