Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma mh Said Thabit mwambungu leo amezikwa katika kijiji cha mwembeni wilayani malinyi ambacho amezaliwa baada ya kufariki dunia siku ya ijumaa tarehe 12/4/2017.
Wakati akitoa salamu za rambirambi waziri wa sera,bunge kazi vijana ajira na walemavu mh Jenista mhagama amesema kuwa kifo cha mwambungu ni pigo kubwa kwani alikuwa ni mhimili mkubwa katika serikakali juu ya utendaji kazi.
Aidha ameongeza kuwa ni vyema kujifunza yale yote mema aliyoyafanya kipindi cha uhai wake juu ya utendaji kazi kwani ni msingi mzuri katika mafanikio.
Naye waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mh William Lukuvi amesema kuwa kuondoka kwa mwambungu ni pengo kubwa kwani alikuwa ni mtu muhimu katika utendaji na kuongeza kuwa msiba huu ni wetu sote na tuamini kuwa kila mtu ana siku yake Ya kuondoka ila haijulikani ni lini.
Said Thabit Mwambungu ameacha mjane mmoja watoto watatu na wajukuu wawili, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo hadi kifo kinamkuta katika hospitali ya muhimbili jijijni Dar es salaam.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.