Mkuu wa wilaya ya Malinyi Mh Mathayo Masele amewaongoza wananchi, watumishi pamoja na
viongozi mbalimbali wa chama na serikali kuadhimisha siku ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar uliozaa jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika kufanya usafi na kuweka alama
kwa kupanda miti katika mipaka ya eneo la mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya
Ndewele, katika kitongoji cha Ndewele kijiji cha Malinyi.
Akizungumza katika zoezi hilo Mh Masele amesema kukamilika kwa mradi huo kutaondoa
changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kuitafuta elimu ambapo kwa sasa wanafunzi
wanaoishi katika maeneo hayo ya Ndewele hulazimika kutembea kwa zaidi ya kilometa ishirini
kwenda katika sekondari za kipingo, Malinyi na Igawa.
Pamoja na hayo Mh Masele ameongeza kuwa kutokana na shule hiyo kuwa na eneo kubwa
hivyo ameiagiza halmashauri ya wilaya kuhakikisha inapanda miti ya michikichi na mikorosho ili
iweze kutumika kama mradi wa shule hiyo pindi itakapokamilika kwa kuiwezesha shule
hiyo kujiongzea kipato pamoja na kutatua changamoto ya mafuta ya kupikia.
Awali akizungumzia maendeleo ya mradi huo kaimu afisa elimu sekondari Bi Pendo Masalu
amesema kwa sasa ujenzi upo katika hatua ya msingi na wanategemea kuanza kupandisha
kuta hivi karibuni ambapo wameanza na ujenzi wa madarasa manane,ofisi mbili pamoja na
matundu ya vyoo ambavyo vyote ujenzi wake unakwenda sambamba.
Kwa mujibu wa bi Masalu ni kwamba jumla ya shilingi milioni mianne na sabini zilizotolewa na
Rais watanzania mama Samia Suluhu Hasan ndizo zinazotumika katika utekelezaji wa mradi
huo kwa awamu ya kwanza ambapo ameongeza kuwa shule hiyo pia itakuwa ya bweni hapo
baadae na hivyo kuwa chachu kwa watoto kufanya vizuri katika masomo yao.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.